
Waziri wa nchi
ofisi ya Makamu wa Rais muungano na mazingira Mh. January Makamba amewataka
viongozi wa taifa wakiwemo vijana kutekeleza kwa vitendo mambo yaliyofanywa na
waasisi wa Taifa kwa kuepuka vitendo vya rushwa pamoja na uchu wa madaraka.
Mh. Makamba
ameyasema hayo leo katika kongamano la kumbukizi ya mwalimu Julius Kambarage Nyerere
iliyofanyika katika Chuo cha kumbukumbu ya mwalimu nyerere na kuhudhuriwa na
viongozi mbalimbali wa serikali.
Waziri makamba
amesema Hayati Baba wa Taifa enzi za uhai wake alijitoa kwa dhati kulitumikia
taifa bila kujali masilahi binafisi huku akipiga vita vitendo vya rushwa,
uonevu, ubinafisi mambo ambayo viongozi wa sasa wanapaswa kutafakari iwapo
wanayafanyia kazi na kuleta maendeleo kwa wananchi.
Kwa upande wake mzee
Joseph Butiku aliewahi kufanya kazi na mwalimu Julius Kambarage Nyerere amesema
taifa linahitaji kuboresha utoaji wa elimu iliyo bora kwa wananchi ili
kurahisisha uendeshaji wa shughuli mbalimbali kwa wananchi pamoja na swala la
taifa kujitegemea ili kukuza uchumi wake.
Nae mwenyekiti wa
bodi ya chuo cha kumbukumbu ya mwalimu nyerere Prf. Mark Mwandosya amesema
mwalimu Nyerere alijua kuwa nchi huendeshwa kwa mipango na kwamba mipango hiyo
ni lazima itekelezwe ikiwa ni pamoja na kuepusha makundi mambo ambayo viongozi
wa sasa wanapaswa kuyaishi.
Kongamano la
kumbukizi ya mwalimu julius kambarage nyerere imeandaliwa na chuo cha kumbukizi
ya Mwalimu Nyerere ikiwa ni kumbukizi ya kuzaliwa kwake mnamo tarehe 13.4.1922
katika wilaya ya Butiama Mkoani Mara.
Na
Pius Jayunga DODOMA
FM
Comments
Post a Comment