Wito umetolewa kwa
viongozi wa kata zote na mitaa
mbalimbali mkoani Dodoma kuhakikisha zoezi la usafi wa mazingira
katika maeneo yao linafanyika kwa ufanisi.
Wito huo umetolewa
na Afisa mazingira wa manispaa ya Dodoma Bw. Dicksoni Kimaro wakati akizungumza
na Dodoma ambapo amewataka viongozi wa ngazi za mitaa na kata kutumia vyeo
vyao ipasavyo kwa kusimamia wananchi ili kuhakikisha mji unakuwa katika hali ya
usafi.
Ametoa wito huo
mara baada ya baadhi ya maeneo mkoani hapa kuonekana kushindwa kuondoa taka
zilizopo katika maeneo yao ambapo wananchi wake wameshindwa kulipia pesa kwa
muda muafaka kwaajili ya kubebewa taka na kupelekwa sehemu husika.
Akizungumzia maeneo
ambayo bado kuna changamoto kubwa katika ulipaji wa pesa kwaajili ya kubebewa
taka miongonui mwao ni mtaa wa FM, SWAY,pamoja na KIKUYU ambapo amewataka
viongozi wa mitaa hiyo kuzichukulia hatua za haraka changamoto hizo ili waweze kukabiliana nazo.
Na kwa upande wake
Afisa Afya Idara ya usafi na mazingira Bw.JOHN STEVEN LUGENDO ameitaka jamii
kuachana na matumizi ya mashimo kwaajili ya kuhifadhia taka na badala yake
watumie vifaa maalmu vilivyowekwa kwaajili ya kuhifadhia taka ili kuepusha taka
kusambaa na kusababisha magonjwa ya mlipuko.
Sanjari na hayo
wananchi wametakiwa kubadilika kuendana na wakati ikiwa ni pamoja na
kushirikiana katika swala zima la usafi wa mazingira pamoja na uhifadhi wa taka katika vyombo vya kuhifadhia
taka na sio kuchimba mashimo kama ilivokuwa kipindi cha nyuma.
Na
ANIPHA RAMADHAN
CHANZO:DODOMA FM
Comments
Post a Comment