Kutokana na idadi kubwa
ya vijana kubainika kuishi na maambukiza ya virusi vya UKIMWI hapa nchini
Katibu wa baraza la taifa la watu wanaoishi na maambukizi ya virusi vya ukimwi
BW,ENOCK MSHUMBUZI amewataka vijana kujenga mazoea ya kupima afya zao.
Akizungumza na Dodoma FM bwana ENOCK MSHUMBUZI
amebainisha kuwa baadhi ya vijana wamekuwa wakisema ugonjwa wa UKIMWI ni kama Malaria na watatumia dawa lakini tatizo kubwa hawako
tayari kwenda kupima kujua afya zao.
Aidha Bwana ENOCK amewataka vijana kuacha kufananisha ugonjwa wa
UKIMWI kama Malaria na kuongeza kuwa
baadhi ya vijana wanaobainika kwenda
kupima lakini hawachukui majibu yao, wanayakimbia kwa kuhofia
kubainika na virusi vya ukimwi.
Kwa upande wao baadhi ya vijana wamekiri kuwa ni kweli hawana
desturi ya kwenda kupima virusi vya UKIMWI kwa kudai jambo la kupima ni gumu na
badala yake wanaamua kuishi bila kupima kutokana na takwimu za vijana kuongoza
kuishi na maambukizi.
Na,Mindi Joseph Dodoma
FM
Comments
Post a Comment