
Naibu
waziri wa Wizara Afya DK FAUSTINE NDUNGULILE ameahindi kuboresha vituo vya kutolea huduma za afya ili kupunguza vifo vya akina mama wajawazito na watoto.
Naibu waziri amebainisha hayo wakati akizungumza katika kongamano
la kisanyansi la wauguzi na wakunga hii leo mjini Dodoma.
Dokt Ndungulile amesema sekta ya afya
bado inakabiliwa na upungufu wa wauguzi pamoja na wakunga na tayari serikali kupitia
sekta ya afya imedhamiria kuleta mabadiliko na kupunguza vifo hivyo.
Ameongeza kuwa katika kupunguza vifo
vya akina mama wajawazito na watoto serikali tayari imeleta mfuko maalumu ambao
utasaindia kuweka vifaa vitavyowasaidia mama wajawazito pindi watakapoenda
hospitali kujifungua.
Amesema sekta ya afya imeweza kupunguza
vifo vya watoto wadogo chini ya umri wa
miaka mitano lakini kwa upande wa akina mama wajawazito bado hawajafanikiwa.
Katika hatua nyingine amebainisha
kuwa kwa mwaka 2015 takwimu zinaonyesha
vifo vya akina mama 556 walipoteza
maisha kwa kila kizazi hai laki moja na eneo hilo bado hawajalifanyia kazi kwa
kiasi kikubwa.
Na,Mindi
Joseph
Dodoma FM
Comments
Post a Comment