Kufuatia uharibifu mkubwa wa
mazingira katika wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma ambao umekuwa ukifanywa
na wakazi wa wilaya hiyo imepelekea wakazi wa baadhi ya vijiji wilayani
humo kukosa huduma ya maji.
Hayo yameelezwa leo
wilayani humo na Mwenyekiti wa Kijiji cha Idilo kilichopo Kata
ya Mazae bw, ROBERT
NJAMASI wakati akizungumza na DODOMA FM kupitia Taswira ya habari.
NJAMASI amesema kuwa hivi
sasa wakazi wa vijiji vya Idilo,Mazae na Chamhawi wamekuwa wakifanya
uharibifu wa mazingira kwa kufyeka miti ikiwa ni pamoja na kulima katika vyanzo
vya maji.
Aidha kutokana na kuwepo kwa
hali hiyo ameiomba Serikali kuongeza faini pamoja na kifungo cha muda mrefu kwa
wananchi watakaobainika kuharibu mazingira ili kukomesha vitendo hivyo.
Kwa upande wake Afisa
Mazingira wa Wilaya ya Mpwapwa,THEODORY MULOKOZI amebainisha kuwa, wameamua
kuchukua hatua ili kumaliza tatizo hilo kwa kuunda kikosi kazi cha wilaya
ambacho kitakuwa na wataalam mbalimbali wa Mazingira akiwemo Mkuu wa wilaya
hiyo.
Hata hivyo Afisa huyo ameiomba
Serikali kutilia mkazo suala la utunzaji wa mazingira hususani katika wilaya
hiyo ambayo imekuwa na vyanzo vingi vya maji lakini vimekuwa haviwanufaishi
wakazi wa Wilaya ya Mpwapwa kutokana na kuviharibu wenyewe.
Nao baadhi ya wakazi wa vijiji
hivyo wamesema kuwa uharbifu huo umekuwa ukichangia kwa kiasi kikubwa changamoto ya ukosefu wa
maji kuwa kubwa katika maeneo yao na wameiomba serikali kulitazama jambo hilo
kwa jicho la tatu ikiwa ni pamoja na kutoa elimu ya utunzaji wa mazingira kwa
jamii.
NAALFREDBULAHYA
DODOMA FM
Comments
Post a Comment