Mamlaka ya mapato mkoa wa Dodoma inatarajia kuzindua rasimi zoezi la
utoaji wa vitambulisho kwa wafanyabiashara wadogo maarufu kama wamachinga kwa
lengo la kuwatambua na kuchangia pato la
taifa ili kuboresha shunghuli za maendeleo.
Akizungumza na Dodoma FM Afisa huduma na elimu kwa mlipa kodi BARNABAS JOHN MASIKA amesema serikali imepitisha sheria hiyo kwa
lengo la kuwatambua wamachinga wote kwa kuwapatia vitambulisho hivyo ili kurahisisha kuwapatia maeneo ya kufanyia
shughuli zao.
BW, MASIKA amesema kwa mujibu wa utaratibu wa serkikali
wamachinga ambao watapewa vitambulisho
wanatakiwa wawe wamekidhi kuwa
na vitambulisho vya taifa [ NIDA].
Kwa upande wao baadhi ya wamachinga wameipongeza serikali
kwa kuanzishisha zoezi hilo ambalo litawapatia fursa ya kufanya biashara zao tofauti
na miaka iliyopita ambapo walikuwa hawana vitambulisho.
Zoezi la uzinduzi huo wa vitambulisho litafanyika rasmi siku
ya ijumaa wiki hii ambalo linatekelezwa na mamlaka ya mapato kwa kushirikiana
na ofisi ya mamlaka ya vitambulisho vya taifa NIDA ,tawala za mikoa na serikali
za mitaa TAMISEMI.
Na,Mindi Joseph,Hadija, Dodoma
Fm
Comments
Post a Comment