
Waziri wa Maliasili
na Utalii Dk, Hamisi Kigwangala
ameliagiza baraza la
wafanyakazi na wakala wa huduma za
misitu Nchini TFS kushirikiana kwa pamoja
kusimamia kikamilifu Rasiliamali za misitu ili kudhibiti Uharibifu unao
tokana na shughuli za kibinadamu.
Akizungumza na
waandishi wa habari mapema leo katika uzinduzi wa Baraza la wafanyakazi na
wakala wa huduma za misitu TFS DK KIGWANGALA
Amesema ili kudhibiti uharibifu wa rasiliamali hizo baraza linatakiwa
kutoa mapendekezo na mikakati ya namna ya kudhibiti uharibifu huo.
DK KIGWANGALA
ameongeza kuwa uchomaji mkaa, uvunaji wa
mbao pamoja na shughuli za kilimo imekuwa ni vyanzo vikuu vinavyopelekea
uharibifu wa misitu hapa nchini.
Katika hatua
nyingine DK KIGWANGALA amesema asilimia 95 ya mikoa yote nchini wananchi wanatumia nishati ya mkaa pamoja na
kuni na kupelekea kiasi kikubwa cha utoroshwaji wa nishati hiyo kwenda nchi
jirani ikiwepo nchi ya Kenya na Sudani
kusini.
Kwa upande waka
Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya huduma za misitu Tanzania Prof ,DOS SANTOS SILAYO
amesema ili kukabiliana na uharibifu wa misitu wanatarajia kupunguza
matumizi ya nishati ya mkaa pamoja na kuchukua hatua kwa wanaofanya
uharibifu wa rasiliamali za misitu.
Na
Mindi Joseph, Mabawa Chanzo Dodoma FM
Comments
Post a Comment