Wananchi wametakiwa
kuzingatia na Kufuata taratibu za matumizi sahihi ya vipodozi na
dawa wanapohitaji huduma hiyo ili
kujikinga na madhara yanayotokana na matumizi yasiyo sahihi kuwa salama kiafya na kuomba ushauri kwa wataalamu pindi wanapohitaji huduma
hiyo.
Akizungumza na DODOMA
FM leo hii Mkurugenzi wa Taasisi ya
Mamlaka ya Chakula na Dawa T F D A, Dokta Englibeti Mbekenga, amesema ni
vyema wananchi wakajenga tabia ya kukagua bidhaa iliyomaliza muda wa kutumika kwa
lengo la kuepuka madhara yatakayo jitokeza.
Dk,
Mbekenga,amesema ni vyema kupata ushauri na kukagua bidhaa ili kujiridhisha
kama bado inastahili kwa matumizi ya binadamu na kuongeza kuwa wamejipanga
kutokomeza bidhaa zisizo faa kwa matumizi na kuwaomba wanchi kutoa taarifa kwa
vyombo husika ikiwepo T F D A.
Aidha Dk, Mbekenga
amesema wanajitahidi kusimamia kikamilifu maeneo ya mipakani na kuzuia bidhaa
zisizofaa vikiwemo vipodozi ili wananchi
wasipate madhara kwani kuna uingizwaji holela wa vipodozi na dawa ambazo
huingizwa nchini kwa njia isiyo sahihi.
Na,
Reuben Mabawa. Chanzo; Dodoma fm
Comments
Post a Comment