Shirika la umeme
tanesco Mkoani Dodoma limewahimiza wateja wake kuendelea kutumia mfumo wa
malipo ya serikali wa GePG wenye lengo la kuwepo kwa uwazi juu ya uendeshaji wa
taasisi za serikali pamoja na matumizi.
Akizungumza na DODOMA
FM mapema hii leo afisa mahusiano wa TANESCO Mkoani Dodoma Innocent Lupenza amesema
mfumo huo umeanzishwa na serikali ambao umezitaka mamlaka zote zilizopo chini
ya serikali kuingia katika mfumo huo kwa lengo la kutambua matumizi yake.
Mfumo huo
hautaathiri mteja yeyote atakayehitaji huduma kwa TANESCO kwa kuwa huduma
itatolewa kama ilivyokuwa awali na kampuni za simu zitaendelea na mauzo ya
umeme kama kawaida.
Ameongeza kuwa
mauzo yote na faini zote zitalipiwa kwa kutumia mfumo huo kwa lengo la kuwepo
uwazi wa matumizi ya taasisi mbalimbali za serikali.
Katika hatua
nyingine amesema tayari Baadhi ya taasisi zimeshaunganishwa kwenye huduma
hiyo ya GePG ikiwa ni TANESCO,TRA,DUWASA,BANK
Pamoja na kampuni za simu na wateja wote
wataenda kununua kama kawaida na tofauti
ya sasa kutakuwa na tozo kwa upande wa simu.
Na,Mindi
Joseph
Dodoma FM
Comments
Post a Comment