Wakazi mkoani Dodoma wametakiwa kushirikiana na idara ya
uhamiaji pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama kwa kutoa taarifa za wahamiaji haramu na kuacha kuwahifadhi
nyumbani watu wasiowajua ili kusaidia kudhibiti wahamiaji haramu kuingia na
kukaa nchini.
Akizungumza na Dodoma FM mapema leo Afisa Uhamiaji wa Mkoa
wa Dodoma PETER J KUNDY amesema Jukumu la idara ya uhamiaji ni kuhakikisha
linafanya usimamizi na udhibiti wa mipaka ya nchi ,utoaji wa hati za kusafiria
kwa raia na hati za makazi kwa wahamiaji na wananchi wanatakiwa kushirikiana na
idara hiyo ili kusaidia kudhibiti wahamiaji hao.
Bwana KUNDY amebainisha kwa mwaka 2017 idara ya uhamiaji kwa kutumia Doria,misako na
kaguzi wamefanikiwa kukamata wahamiji
haramu 70 Raia wa nchi za Ethiopia,Bururndi,China,Kongo,Kenya,India pamoja na
Malawi na kuchukuliwa hatua mbalimbali.
Katika hatua nyingine ameongeza kuwa wamiliki wa vyombo vya
usafiri wanatakiwa kuhakikisha vyombo vyao vya usafiri havitumiki kusafirisha
wahamiaji haramu pamoja na wamiliki wa shule binafisi kuhakikisha waalimu na
raia wa kigeni watakao waajiri wana vibali kutoka idara ya uhamiaji na wizara
ya kazi.
Takwimu zinaonesha kwa mwaka 2018 kuanzia January hadi march
watuhumiwa waliokamatwa ofisi ya uhamiaji mkoa wa Dodoma jumla ni 103 huku Ethiopia
ikiongoza kwa wahamija haramu kuingia nchini.
Na,Mindi Joseph,Hadija Chanzo: Dodoma FM
Comments
Post a Comment