Taasisi za serikali
na binafsi zimeombwa kuhakikisha zinatengeneza mazingira rafiki ya utendaji
kazi kwa watu wenye ulemavu ili kuwasaidia kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.
Wito huo umetolewa
leo na afisa mipango kutoka katika taasisi ya HOPE DELIVERY FOUNDATION Bi, Beatrice Magoda wakati akizungumza na Dodoma FM kupitia kipindi cha Taswira ya habari ambapo amesema kuwa taasisi zote na jamii kwa ujumla
zinatakiwa kuangalia suala la kutengeneza miundombinu rafiki kwa walemavu ili
kuwaondolea changamoto ambazo zimekuwa zikiwasababisha kushindwa kufanya kazi
kwa ufanisi.
Amesema kuwa wapo
baadhi ya watu wenye ulemavu ambao
wameajiriwa katika ofisi mbalimbali wamekuwa wakipata taabu katika utendaji
kazi wao na wakati mwingine hata kuchelewa kufika kazini ili kuanza majukumu
yao jambo ambalo husababisha kazi wanazozifanya kuwa ngumu.
Aidha amevikumbusha
vyombo vya habari kutumia njia rahisi na rafiki kwa
walemavu kufikisha taarifa mbalimbali ili kuwasaidia kutambua mambo muhimu
yanayoihusu jamii ili kuwasaidia katika utekelezaji wa majukumu yao.
NA ALFRED BULAHYA DODOMA
FM
Comments
Post a Comment