TAASISI YA HOPE DELIVERY FOUNDATION YASEMA UKATILI KWA WATU WENYE UALBINO HUTOKEA ZAIDI MIAKA MIWILI KUELEKEA UCHAGUZI
Watanzania
wametakiwa kuachana na imani potofu za kuwaua watu wenye Ualbino kwa madai ya kujipatia
vyeo mbalimbali.
Rai hiyo imetolewa
na Mkurugenzi wa Taasisi ya Hope Delivery Foundation Michael Salali wakati
akizungumza na Dodoma FM mapema leo.
Kwa mujibu wa Bwana
Salali amesema kutokana na tafiti zao inaonyesha kuwa matukio mengi ya ukatili
dhidi ya watu wenye ualbino hutokea ndani ya miaka miwili kuelekea uchaguzi mkuu.
Bw. Salali amesema hivi karibuni kulitokea ukatili kwa msichana
mwenye ualbino ambaye alifanyiwa ukatili wa kunyolewa nywele zake pamoja na kukatwa kucha na mganga ambae
alipelekwa na jirani wa familia hiyo huko wilayani Tarime.
Hata hivyo ukatili
dhidi ya watu wenye ualbino umeonekana kuwa chanzo kikubwa ni waganga wa
kienyeji ambao huwadanganya watu wenye mahitaji yao binafsi kwa kuwataka walete
viungo vya Albino ili waweze kuitimiziwa haja zao.
Bwana Salali
amesema Taasisi ya Hope Delivary Foundation anayosimamia inapaza sauti kwa
jamii kwa kuitaka itambue kuwa tofauti ya watu wenye ualbino ya ngozi ni Rangi
na si vinginevyo kama wanavyoaminishwa na waganga wa kienyeji.
Na ANIPHA RAMADHAN CHANZO:DODOMA
FM
Comments
Post a Comment