
Katika kuelekea
kwenye maadhimisho ya miaka 54 ya
muungano wa Tanganyika na Zanzibar imeelezwa kuwa licha ya kuwepo kwa mafanikio ya kisiasa pia
mwananchi mmoja mmoja anafaidika katika kuinuka kiuchumi pamoja na kupata
nafasi ya kumiliki ardhi katika pande zote mbili.
Kaimu mkurugenzi Idara ya Muungano Ofisi ya
Makamu wa Rais Bw,Sifuni Joshua Msangi
amesema muungano umesababisha wananchi kunufaika kwa kumiliki ardhi na kufanya
shughuri za kilimo na uwekezaji pamoja na utaliii kwa wananchi wa Tanzania bara pamoja na Zanzibar.
Amesema serikali ya
jamuhuri ya muungano wa Tanzania imekuwa ikifanya shughuri nyingi katika
kuwawezesha wananchi wa pande zote mbili kushiriki katika shughuri za
uzalishaji zinazowawezesha wananchi kuinuka kiuchumi ikiwemo katika miradi ya
kilimo.
Kwa upande wao
baadhi ya Wananchi wamesema kuwa muungano umekuwa na faida nyingi katika maisha
yao ya kila siku ikiwemo kuimarisha ulinzi na usalama katika jamii, kuwepo kwa
amani na upendo katika pande zote mbili.
Maadimisho ya miaka
54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
yanatarajiwa kuadhimishwa mkoani hapa
huku kauli mbiu ikiwa ni MUUNGANO WETU NIWAMFANO DUNIANI TUUENZI,
TUULINDE, TUIMARISHE NAKUUDUMISHA KWA MAENDELEO YA TAIFA LETU
Na
Phina Nimrod Chanzo:Dodoma Fm
Comments
Post a Comment