
Serikali
kupitia wizara ya mambo ya ndani ya nchi imezindua rasmi mfumo wa utoaji hati
za kisasa za kusafiria kwa njia ya kielectroniki ikiwa ni miongoni mwa hatua za
kuendelea kupunguza uhalifu unaofanywa na watu
mbalimbali wakiwemo wahamiaji haramu hapa nchini.
Zoezi hilo limezinduliwa mapema hii
leo Jijini Dodoma na waziri wa mambo ya ndani Mwigulu Nchemba na kuwataka
wananchi watakaopatiwa hati hizo kuhakikisha wanatunza kikamilifu ili
kuepusha kutumiwa na wahalifu mbalimbali.
Amesem kuwa ni vyema wananchi
wakatambua umuhimu wa kuwa na hati hizo ili kuepusha usumbufu unaoweza
kujitokeza kama kuhusishwa na mambo ya kihalifu kwani kuna baadhi ya watu ambao hupata pasipoti kwa
njia ya mkato na kwenda kuzifanyia uhalifu katika nchi za nje kitu ambacho kinaidhalilisha
Tanzania.
Pamoja na hayo amesema, uzinduzi huo
una lenga kukidhi matakwa ya usalama wa nchi na viwango vya kimataifa na kwamba
pasipoti hizi zimetengenezwa kwa teknolojia ya kisasa na zitakuwa na uwezo wa kubeba taarifa za
mwombaji bila kugushi na amesema pasipoti za zamani zitaendelea kutumika hadi
mwezi January mwaka 2020 .
Kwa upande wake kamishina Jenerali
wa uhamiaji Dkt.Anna Peter amesema kuwa pasipoti hizo zitatumika kwa kipindi
cha miaka kumi ambapo gharama yake ni sh.laki moja na nusu serikali ina mpango
mkakati wa kueneza zoezi hili nchi nzima ili kuwafikia wananchi wote na kwamba
kila atakayekuwa na pasipoti atakuwa na nakala ya pasipoti hiyo kwenye simu
yake ya kiganjani.
Sambamba na hayo ametaja idadi ya
pasipoti ambazo zimekwisha kutolewa kwa wananchi tangu Rais wa Jamhuri ya
muungano wa Tanzania azindue zoeli hili mwezi January mwaka huu jijini Dar es
Salaam kuwa ni 10863.
Na Alfred Bulahya Dodoma
FM
Comments
Post a Comment