
Waziri
Mkuu Kasimu Majaliwa amesema lengo la kuzuia biashara ya mazao ya chakula kwenda
nje ya nchi ikiwemo zao la mahindi lililenga kupunguza tatizo la upungufu wa
chakula pamoja na kuimarisha viwanda vya ndani kupata mapato.
Mh.
Kasimu Majaliwa ameyasema hayo leo Bungeni Mjini Dodoma katika kipindi cha
maswali ya papo kwa hapo kwa Waziri Mkuu wakati akijibu swali la Mbunge Aidan
Khenan aliehoji ni lini Serikali itaruhusu mazao ya chakula kuuzwa nje ya Nchi.
Waziri
Mkuu amesema baada ya Serikali kuzuia mazao hayo kuuzwa nje ya Nchi imesaidia
kupunguza tatizo la njaa kwa wananchi na kutokana na mvua zinazoendelea
kunyesha kwa msimu huu huwenda ikasaidia kupatikana kwa chakula cha kutosha na
hivyo kufungua fursa ya soko la mazao hayo nje ya nchi.
Aidha
Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa amesema Serikali imefanya jitihada za kuboresha
sekta ya kilimo kwa kutoa pembejeo za kilimo kulingana na uhitaji, mbolea na
madawa pamoja na kuimarisha kilimo cha kitaalamu ambacho kitasaidia kuzalisha
zao la mahindi kwa wingi.
Katika
hatua nyingine Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa ametoa wito kwa wananchi kuzitumia
ipasavyo mvua zinazoendelea kunyesha kwa kulima mazao ya biashara ikiwemo
mahindi, pamba, kahawa, chai na Serikali itashirikiana kwa karibu na wakulima
hao kutafuta fursa za masoko.
Na Pius Jayunga Dodoma FM.
Comments
Post a Comment