
Serikali kupitia wizara ya fedha na mipango imetolea ufafanuzi juu ya
hoja ya kuto kuonekana kwa matumizi ya Serikali ya kiasi cha Trilioni 1.51
kutokana na ripoti ya mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za Serikali (CAG).
Naibu Waziri wa fedha na mipango Dr. Ashantu Kijaji ametoa ufafanuzi huo
leo Bungeni mjini Dodoma wakati akitoa kauli rasmi ya Serikali juu ya fedha
kiasi cha trilioni 1.51 zinazodaiwa kuto kuonekana matumizi yake.
Amesema katika kipindi cha mwaka 2012/13 hadi 2016/17 Serikali kupitia Wizara
ya fedha ilikuwa katika kipindi cha mpito cha miaka mitano ya mpango mkakati wa
kuandaa hesabu za Serikali kwa kutumia mfumo wa viwango vya kimataifa vya
uhasibu katika sekta ya umma.
Naibu
Waziri Dr. Ashantu Kijaji amesema katika taarifa ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa
hesabu za Serikali CAG imeeleza jumla ya mapato ya Serikali kwa mwaka 2016/17
yalikuwa trilioni 25.3 fedha hizo zikijumuisha mapato ya kodi, mapato yasiyo ya
kodi mikopo ya ndani na nje ikiwemo misaadsa
na mikopo nafuu kutoka kwa washirika wa maendeleo.
Ufafanuzi huo
unakuja ikiwa ni siku chache baada ya mwenyekiti wa chama cha ACT Wazalendo Mh.
Zitto Kabwe alizungumza na vyombo vya habari na kueleza kuwa katika ukurasa wa
34 wa ripoti ya mkaguzi na mdhibiti mkuu
wa hesabu za Serikali CAG kunaonesha kiasi cha sh. Trilioni 1.51 hazikutolewa
kwa matumizi wala kukaguliwa.
Na Pius Jayunga Chanzo: Dodoma FM
Comments
Post a Comment