
Serikali imesema azma ya kusisitiza ujenzi wa viwanda Nchini
ni kuhakikisha kuwa inachochea mageuzi ya kiuchumi ili ifikapo mwaka 2025 Tanzania
iwe imefikia uchumi wa kati.
Waziri wa viwanda biashara na uwekezaji Mh. Charels Mwijange
ameyasema hayo leo wakati akihutubia wananchi na viongozi mbalimbal wa Serikali
katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi wa ujenzi wa kiwanda cha kemikali cha
Msufuni Mkoani Pwani.
waziri Mwijage amesema lengo la kufikia uchumi wa kati ni kumsaidia kila
mtanzania kuwa na uhakika wa kupata kipato cha kutosha kinachomuwezesha kumudu
gharama za maisha pamoja na kuendesha shughuli nyingine za maendeleo na azma
hiyo itafanikiwa iwapo uwekezaji katika sekta ya viwanda utapewa kipaumbele.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Eng. Evarist Ndikilo amesema ujio
wa kiwanda hicho Mkoani Pwani ni mwendelezo wa kujengwa kwa viwanda vingi Mkoani
hapo na baada ya kukamilika kikawanda hicho kutasaidia katika swala la
upatikanaji wa dawa za kutibia maji ndani ya Nchi.
Kwa upande wake afisa mtendaji mkuu wa taasisi ya SELBA Dr.
Karim Abdalah amesema wamedhamiria kukamilisha mrad huo na kusaidia katika upatikanaji
wa mahitaji muhimu ya kutibu maji pamoja na kuongeza fursa ya ajira hasa kwa
raia wa Tanzania.
Na Pius Jayunga Dodoma FM
Comments
Post a Comment