Serikali imedhamiria kuendelea kuboresha ufundishaji wa masomo ya sayansi ili kuongeza idadi ya wasomi waliobobea katika masomo ya sayansi.
Naibu
Waziri wa elimu sayansi na teknolojia Mh. Tate Ole Nasha ameyasema hayo leo
Bungeni Mjini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa jimbo la Bunda Mjini Ester Bulaya alietaka kufahamu ni kwa
kiasi gani tatizo la upungufu wa walimu wa masomo ya sayansi limeweza kutatuliwa.
Amesema
Serikali imekwisha kuchukua hatua mbalimbali ikiwemo kuimarisha ufundishaji wa masomo
ya sayansi na hisabati, ambapo wahitimu 1799 wa kundi la kwanza watahitimu
masomo yao ifikapo mwezi wa 5, 2018 kundi la pili likiwa na wahitimu 5401 ambao
wanatarajiwa kuhitimu ifikipo mei, 2019.
Hata
hivyo Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini Ester Bulaya amesema katika Jimbo lake
kuna uhaba mkubwa wa walimu wa masomo ya sayansi hatua inayochangia wanafunzi
katika Wilaya hiyo kufanya vibaya katika masomo yao huku Naibu Waziri wa elimu Mh.
Tate Ole Nasha akisema changamoto hiyo ni
kwa Nchi nzima .
Katika
hatua nyingine Naibu Waziri Tate Ole Nasha amesema Serikali haitarajii kuwarudisha
shuleni wanafunzi waliobebeshwa ujauzito wakiwa shuleni na kwamba kufanya hivyo
ni sawa na kuhamasisha vitendo vya ngono kwa wanafunzi na hii ni kufuatia swali la Mbunge Rehema Migige aliehoji ni lini
Serikali itawarejesha masomoni wanafunzi walio bebeshwa ujauzito.
Na PIUS JAYUNGA
DODOMA FM
Comments
Post a Comment