
Wizara ya ujenzi uchukuzi na mawasiliano kwa kushirikiana
na jeshi la polisi Nchini wameanzisha utaratibu maalumu utakaosaidia kuimarisha
usalama wa wananchi katika matumizi ya mitandao.
Naibu waziri wa ujenzi uchukuzi na mawasiliano Eng.
Atashasta Nditiye ameyasema hayo leo Bungeni Mjini Dodoma wakati akijibu swali
la Mbunge wa Jimbo la Busokelo Mh.
Atupele Fredy Mwakibete aliehoji Serikali imejipangaje kukabiliana na vitendo
vya wizi wa mitandao kwa wananchi.
Naibu Waziri Nditiye amesema hatua zilizokwisha kuchukuliwa na Serikali ni
pamoja na matumizi ya sheria ya makosa ya mtandao na miamala ya kielekroniki iliyotungwa mwaka 2015 kwa lengo
la kutambua miamala inayofanyika kimtandao yakiwemo pia makosa na kuchukua
hatua sitahiki pale yanapotokea makosa hayo.
Eng. Nditiye amekiri kuendelea kwa vitendo vya wizi
pamoja na uhalifu wa mtandaoni na hatua zinazoendelea kufanyika ili kukomesha
vitendo hivyo ni pamoja na kutengeneza program zinazoweza kumaliza tatizo hilo
sambamba na kuwapeleka wataalamu wa maswala ya tehema kujifunza katika Nchi
zilizoednelea ikiwemo Israel, India Na Marekan.
na Pius Jayunga Dodoma FM
Comments
Post a Comment