
Serikali ya mkoa wa Dodoma kwa kushirikiana na wadau wengine vikiwemo vyombo
vya habari wamendelea na jitiada za kutoa elimu juu ya kujikinga na ugonjwa wa
kipindupindu ili kudhibiti kuongezeka ugonjwa huo.
Akizungumza na
Dodoma FM Mganga Mkuu wa mkoa wa Dodoma Doctor JEMES KIHOLOGWE amesema kuwa serikali
ya mkoa kwa kushirikiana na wadau
wengine wanaendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu tahadhari za kuchukua
kujikinga na ugonjwa huo.
Licha ya hivi
karibuni mkoa wa Dodoma kuripotiwa kuongoza kwa uwepo wa ugonjwa wa
kipindupindu DOKTA KIHOLOGWE amesema hii inatokana na takwimu ya wagonjwa
waliopatikana kutoka vijiji vya wilaya za mpwapwa na chamwino huku akisema kuwa
kwa upande wa manispaa ugonjwa huo umepungua.
Aidha Doctor Kihologwe
amesema mara tu baada ya kuripotiwa kuwepo wagonjwa wa kupindupindu huko
mpwapwa na chamwino tayari mamlaka husika imepeleka DAWA ZA KUTIBU MAJI na kuongeza
kuwa halmashauri ya kila wilaya kwa kushirikiana na serikali za mitaa
wanaendelea kushughulikia suala hilo.
DoctorKIHOLOGWE amewataka
wananchi kutotumia maji ya kwenye makolongo na mabwawa na kuzingatia njia za tahadhali
juu ya kujikinga na ugonjwa huo hatari.
Na
RWEIKIZA KATEBALIRWE DODOMA FM
Comments
Post a Comment