
Ili kufikia azma ya Tanzania ya viwanda Sekta ya kilimo kupitia kwa afisa kilimo
mkoani Dodoma imeahidi kuendelea kuboresha sekta hiyo ikiwa ni pamoja na
kuongeza wataalamu wa kilimo.
Hayo yamebainishwa
na Afisa Kilimo wa mkoa wa DODOMA Bwana BERNARD ABRAHAM wakati akizungumza na Dodoma FM mapema hii leo
juu ya namna ambavyo Mkoa wa Dodoma kupitia sekta ya kilimo umejipanga.
Afisa Kilimo huyo amekiri
changamoto iliyopo katika sekta ya kilimo ni upungufu wa maafisa kilimo katika
baadhi ya kata.
Bwana Abraham
amesema kuwa kutokana na wananchi wengi kujikita kwenye Kilimo na kupelekea
wengi kupata ajira ni vyema kilimo kikapewa
kipaumbele kwa kuwepo watumishi wa kutosha ili kuwasaidia wakulima.
Katika hatua
nyingine amebainisha kuwa hakuna sekta inayojitosheleza kwa wafanyakazi na
watumishi waliopo watasaidia kwa kipindi hiki mpaka serikali itakapoongeza watalaam
wengine.
Aidha wakulima
wanatakiwa kutumia kilimo cha kisasa kitakachowaletea manufaa hususani vijijni
ambapo bado hawazingatii wakidai kilimo cha kisasa kinaharibu mashamba yao.
Na,Mindi
Joseph Chanzo: Dodoma FM
Comments
Post a Comment