Sekta
ya kilimo Mkoani Dodoma bado inakabiliwa na changamoto ya upungufu wa maafisa
ugani hali ambayo imepelekea kushindwa kuwahudumia vyema wakulima.
Hayo yamebainishwa
na mjumbe wa JUWACHA BRAITONI MWIDOWE ambapo amesema maafisa ugani wamekuwa
wachache ukilinganisha na idadi ya wakulima kuwa wengi huku maafisa waliopo
wakiwa hawana vitendea kazi vya kuwawezesha kuwafikia wakulima wote.
Afisa kilimo Mkoa
wa Dodoma Bwana BERNARD ABRAHAM amekiri ni kweli maafisa ugani ni wachache
kutokana na wingi wa wakulima.
Bwana Abraham
amewataka wakulima wasisuburi Maafisa wawatembelee bali wao watoe taarifa pindi
mazao yanaposhambuliwa na wadudu ili kuweza kusaidiwa kwa wakati.
Na,Mindi Joseph
Dodoma Fm
Comments
Post a Comment