
Rais
Dr. John Pombe Magufuli amesema mwitikio wa wananchi katika swala la ulipaji wa
kodi unachangia kwa kiasi kikubwa kufanikisha Ujenzi wa miundombinu zikiwemo
barabara.
Rais
Magufuli ameyasema hayo leo wakati akizungumza na wananchi Wilayani Kondoa katika
uzinduzi wa barabara kutoka Kondoa Jijini Dodoma hadi Babati Mkoani Manyara kwa
kiwango cha lami yenye urefu wa kilomita 251.
Amesema
ujenzi wa barabara hiyo umegharimu kiasi cha shilingi Bil. 378.4273 ambapo Serikali
kupitia kodi za wananchi imechangia shilingi Bil. 107.654, Bank ya maendeleo ya
Afrika ikitoa mkopo wa shilingi bilioni 203.14 na kiasi cha shilingi bilioni
67.62 kikitolewa na Serikali ya Japan ili kufanikisha ujenzi huo.
Rais Magufuli amewataka
wananchi na hasa wakazi wa Wilaya ya Kondoa Jijini Dodoma kuitunza ipasavyo miundombinu
hiyo ya barabara na kuwasihi waendeshaji wa vyombo vya moto kuepuka mwendo kasi
ili kuokoa maisha ya watanzania.
Kwa
upande wake waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amesema
licha ya barabara hiyo kuunganisha Mikoa ya Dodoma na Manyara pia ni sehemu ya
babarabara kuu inayounganisha Nchi tisa za Africa ambazo ni Africa Kusini, Botswana, Zimbabwe,
Zambia, Tanzania, Kenya, Ethiopia pamoja na Sudan Kusini.
Na Pius Jayunga Dodoma FM
Comments
Post a Comment