
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr.
John Pombe Magufuli amewataka wanasheria Nchini kusimamia ipasavyo sheria za
nchi katika kudhibiti vitendo vya baadhi ya watu wanaotumia mitandao ya kijamii
kwa kutoa takwimu za kupotosha umma.
Rais Magufuli ameyasema hayo leo Ikulu Jijini
Dar Es Salaam wakati akiwaapisha majaji 10 Naibu
Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka pamoja
na Naibu Wakili wa Serikali walioteuliwa
na Rais Magufuli hivi
karibuni.
Rais Magufuli amewataka wanasheria pamoja na
majaji kuzishughulikia mapema kesi za watu wanaotuhumiwa kujihusisha na utoaji
wa taarifa za uongo katika mitandao ya kijamii na hatimae kupotosha umma wa
watanzania juu ya taarifa rasmi zinazotolewa na Serikali.
Kwa upande wake waziri wa katiba na sheria
prof. Paramagamba Kabudi amesema katika kipindi hiki kesi nyingi zimeibuka na
hii ni kutokana na nchi za Afrika zinapochukua maamuzi ya kufanya maendeleo kwa
wananchi hujuma nazo huongezeka ili kukwamisha jitihada hizo.
Akifafanua utaratibu wa kuchanguliwa kwa majaji
hapa nchini Jaji mkuu wa tanzania Prof. Ibrahimu Hamis Juma amesema ili kuondoa
hujuma na taarifa za upotoshaji mitandaoni tume hutoa nafasi kwa wadau wa
sheria kutoa majina ya watu wanaoweza kukidhi matakwa ya katiba na walio na
uwezo wa kufanya shughuli za ujaji.
Na Pius Jayunga Chanzo: Dodoma FM
Comments
Post a Comment