Rais
wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli leo ametangaza rasmi
kuupa hadhi ya Jiji Mkoa wa Dodoma kutoka ngazi ya Manispaa.
Rais
Magufuli ametangaza uamzi huo wakati akihutubia wananchi katika maadhimisho ya
miaka 54 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar maadhimisho yaliyofanyika katika
uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma.
Wakati huo huo aliekuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Bw. Godwin Kunambi amepandishwa hadhi na kuwa Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma.
Rais Magufuli amesema
azma ya Serikali kuhamia makao makuu ya Nchi Dodoma haitarudi nyuma na tayari
watumishi zaidi ya 3800 wameshahamia Dodoma ambapo ameagiza maandalizi yote ya
kisheria kufanyika mapema.
Mh Magufuli amewahakikisha watanzania kuwa Serikali ya awamu ya tano itaendelea
kuuenzi muungano na kuwataka wananchi kudumisha upendo, umoja na mshikamano
huku akieleza baadhi ya mambo yaliyofanikiwa katika Serikali ya awamu ya tano
kuwa ni pamoja na kukua uchumi kwa asilimia 7 na kupunguza maambukizi ya
ugonjwa wa malaria kutoka asilimia 14.3 hadi asilimia 7.3%.
Baadhi
ya wakazi wa Mkoa wa Dodoma wakizungumza na Dodoma FM kwa nyakati tofauti
wamesema Muungano wa Tanganyika na Zanzbar umeleta mafanikio makubwa Nchini
hasa katika kudumisha amani, upendo, mshikimano sambamba na viongozi wakiwemo
wananchi kila mmoja kuwajibika kwa nafasi yake ili kuleta maendeleo Nchini.
Maadhimisho
ya sherehe za muungano wa Tanganyika na Zanzibar yamefanyika leo hapa Jijini
Dodoma mgeni rasmi akiwa Rais na amiri jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na
usalama Nchi Rais Dr. John Pombe Magufuli huku maadhimisho hayo yakibebwa na
kaulimbiu isemayo miaka 54 ya Muungano wetu ni mfano wa kuigwa Duniani,
tuuenzi, tuulinde na kuudumisha kwa maendeleo ya Taifa letu.
Na Pius Jayunga Dodoma
FM
Comments
Post a Comment