
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amesema licha ya
kupiga hatua katika uzalishaji wa nishati ya umeme nchini bado wananchi
wanalazimika kutumia nishati ya mkaa, kuni na mafuta ya taa.
Rais Magufuli
ameyasema hayo leo wakati akizindua Mtambo
wa Kufua Umeme wa Kinyerezi II uliopo katika jimbo la segerea Jijini Dar es
salaam na kueleza kuwa kuna haja ya kuendelea kuzalisha nishati ya umeme zaidi
ili kutosheleza mahitaji ya watanzania.
Amesema kwa mujibu
wa utafiti uliofanywa na ofisi ya takwimu kwa mwaka 2015/16 inaonesha asilimia
36.6 ya watanzania ndio waliounganishwa na huduma ya nishati ya umeme na
waliobaki wakiwa wanatumia nishati ya mkaa, kuni pamoja na mafuta katika
matumizi yao.
Rais Magufuli amesema
kutokana na matumzi ya nishati ya kuni na mkaa yamechangia kwa kiasi kikubwa
uharibifu wa mazingira ambapo kila mwaka hekta 400 elfu za misitu zinaharibiwa
kutokana na ukatiji wa miti pamoja na madhara ya kiafya hivyo ni lazima
uzalishaji wa nishati ya umeme uendane sambamba na mahitaji ya idadi ya
watanzania.
Nae Waziri wa nishati Dr.
Medard Kaleman amesema katika kipindi cha miaka mitatu ijayo eneo la kinyerezi
litakuwa na uwezo wa kuzalisha umeme mega wati 1692 kutokana na jitihada zinaendelea
kufanyika katika kukamilisha miradi iliyosalia.
Mradi wa kufua
umeme wa kinyerezi II uliozinduliwa leo na Rais Dr. John Pombe Magufuli
unatarajiwa kuzalisha umeme wa mega watt 240.
Na Pius Jayunga Dodoma FM
Comments
Post a Comment