Katibu
wa Elimu Chama cha Wafanyakazi RAAWU Makao makuu Bwana Ramadhan Mwendwa ameishukuru serikali kufuatia
agizo lake kurudishwa kazini kwa
watumishi wote wa Umma waliofukuzwa kimakosa ikiwemo wale walioishia darasa la
saba.
Katibu huyo ambae awali
alikuwa Katibu wa chama cha wafanyakazi RAAWU kanda ya kati na Katibu wa TUCTA
Mkoa wa Dodoma amesema hayo wakati
akiongea na Dodoma FM ambapo amebainisha kuwa awali wakati akiwa katibu wa
chama hicho kanda ya kati alijitahidi kupigania suala hilo ikiwepo kupeleka kwa
viongozi wa ngazi za juu.
Bwana Mwendwa amesema kitendo cha serikali
kuwarudishia mishahara yao itasaidia kupunguza machungu yao wakati walipokuwa
wametolewa kwenye nafasi zao.
Amewashauri viongozi wa chama cha
wafanyakazi ngazi za chini kuhakikisha wanatetea maslahi ya wafanyakazi na Taifa
kwa ujumla.
Kwa upande wake Bwana Omary Shaibu amesema
serikali imefanya maamuzi ya busara kwani wengi wao walikuwa wana ujuzi mzuri.
Hapo jana katika kikao
cha bunge Serikali kupitia Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora George Mkuchika aliagiza kurudishwa kazini watumishi
wote wa Umma waliofukuzwa kimakosa ikiwemo wale walioishia darasa la saba walio ajiriwa
Serikalini kabla ya tarehe 20 mwezi mei mwaka 2004.
Na
Benard Filbert Dodoma
FM
Comments
Post a Comment