Naibu
Waziri wa afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Dr. Faustine Ndugulile
amesema mpaka sasa bado haijapatikana dawa rasmi inayoweza kutibu ugonjwa wa
kisukari licha ya tafiti mbalimbali zinazoendelea kufanyika.
Dr.
Faustine ametoa ufafanuzi huo leo Bungeni Mjini Dodoma wakati akijibu swali la
Mbunge wa viti maalumu Dr. Christine Gabriel Ishengoma aliehoji Serkali ina mpango
gani kufanya utafiti kuhusu dawa za kutibu ugonjwa huo.
Naibu
Waziri wa Afya amesema mpaka sasa Duniani kote bado haijapatikana dawa
inayoweza kutibu ugonjwa wa kisukari na kinachofanyika kwa sasa ni mgonjwa
kupatiwa matibabu ya kiwango bora cha kumuwezesha kuishi ili kuvilinda viungo
vingine visiathiriwe.
Amesema
pamoja na tafiti zinazoendelea kufanyika Duniani ili kufanikisha upatikanaji wa
dawa zitakazokuwa na uwezo wa kutibu ugonjwa wa kisukari zinajumuisha tafiti za
kutengeneza seli za kongosho na kisha kuzipandikiza na baada ya tafiti hizo
kukamilika na kuleta mafanikio serikali ya Tanzania itahakikisha huduma hiyo
inapatikana hapa Nchini.
Katika
hatua nyingine Dr. Faustine ametoa rai kwa wananchi wakiwemo wazazi kuzingatia
misingi ya lishe kwa watoto wao ili kuepusha uzito uliopitiliza, kufanya mazoezi
ya mara kwa mara hatua inayoweza kusaidia kujiepusha na ugonjwa huo.
Na Pius Jayunga Dodoma FM Radio
Comments
Post a Comment