Mkuu wa Mkoa wa
Dodoma, Dk Binilith Mahenge amesema kuna ubadhirifu wa Sh1.5 bilioni kwenye
mradi wa maji katika wilaya za Kondoa na Chemba ambao unasuasua.
Dk Mahenge amesema
hayo leo Aprili 27 Kondoa, Dodoma wakati wa hafla ya uzinduzi wa barabara ya
Kondoa – Babati yenye urefu wa kilomita 251 inayozinduliwa na Rais John
Magufuli.
Mkuu huyo wa mkoa
amesema mradi huo ulitengewa Sh2.8 bilioni kwa ajili ya wilaya hizo lakini
kulitokea ubadhirifu wa Sh1.5 bilioni. Amebainisha kwamba vyombo vya dola
vinaendelea na uchunguzi wa ubadhirifu huo.
“Tayari vyombo vya
dola vinafanya uchunguzi wa ubadhirifu wa fedha hizo. Dhamira ya Serikali iko
pale pale kuhakikisha kwamba maji yanapatikana katika mkoa wa Dodoma,” amesema
mkuu huyo wa mkoa.
Dk Mahenge amesema
Serikali imetenga Sh70 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu katika mkoa
huo. Amesema kwenye sekta ya maji, Serikali imeanza ujenzi wa visima vitano
ambavyo vitasaidia kukidhi mahitaji ya maji katika mkoa huo.
Dodoma FM
Comments
Post a Comment