Halmashauri ya
manispaa ya Dodoma imesema imeweka mpango kabambe wa Mji wa Serikali unaotarajiwa
kukamilika baada ya miaka kumi.
Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma Godwin kunambi amesema halmashauri imetekeleza maagizo yaliyotolewa
na Rais Magufuli na kwamba katika mji huo yametengwa maeneo mbalimbali yakiwemo
ya makazi, viwanda vidogovidogo, barabara pamoja na biashara.
Kunambi amesema ili
kukamilika kwa ujenzi huo wa Mji wa Serikali gharama zitahitajika fedha za
kitanzania shilingi Trilioni kumi na kwamba tayari mabalozi kutoka nchi
mbalimbali wameshaanza kufika kwa ajili ya kupatiwa viwanja.
Amesema dhumuni la
kufanya hivyo ni kuufanya Mji uendane na mabadiliko ya Mji, ukuaji pamoja na
ongezeko kubwa la wananchi Mkoani Dodoma.
Na
Phina Nimrod Chanzo:Dodoma
FM
Comments
Post a Comment