Naibu waziri wa
afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Dr. Faustine Ndugulile amesema
Serikali inatambua kuwepo kwa ongezeko la vifo vya mama na mtoto huku
ikiendelea na mikakati mbalimbali inayolenga kupunguza vifo hivyo.
Dr. Ndugulile
ametoa kauli hiyo leo Bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge
Halima Abdalha Bulembo alietaka kufahamu Serikali ina mkakati gani kupunguza
vifo vya mama pamoja na watoto hasa kwa watoto njiti.
Amesema mkakati
unaondelea kwa sasa ni pamoja na kuboresha vituo vya afya Nchini katika vituo
vya dharula, kuweka mkakati wa huduma za watoto njiti na watoto waliozaliwa
katika kipindi maalumu, zinapatikana katika hospitali zote zikiwemo hospitali
za Wilaya, Mkoa na Rufaa.
Kwa upande wake
Naibu waziri wa Tamisem Mh. Joseph Sinkamba Kandege amesema Wizara imetenga
kiasi cha shilingi mil. 22.1 kwa mwaka wa fedha 2018/19 kwa ajili ya kutolea
mafunzo maalumu ya kumsaidia mtoto njiti na hadi sasa kumekuwepo na mashine za
aina tatu zinazo weza kuwasaidia watoto wachanga kupumua.
Kwa mjibu wa ripoti
iliyochapishwa mwaka 2012 na jopo la wataalamu wa wakilishi wa mashirika ya
umoja wa Mataifa, Nchini Tanzania takwimu zinaonesha asilimia 13 ya watoto
huzaliwa wakiwa na uzito pungufu ambao huchangia kwa asilimia 86 ya vifo vya
watoto wachanga.
Na Pius Jayunga Dodoma FM
Comments
Post a Comment