
Serikal
imesema itaendelea kuhakikisha inapambana na kila aina ya mianya inayotumika
katika kusafirisha dawa za kulevya wakiwemo pia watumiaji wa dawa hizo.
Naibu
Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri mkuu kazi vijana na ajira Mh. Anthony Mavunde
ameyasema hayo leo Bungeni Mjini Dodoma wakati akitolea ufafanuzi hatua
zinazochukuliwa na Serikali ili kukabiliana na wale wanaoendelea na biashara
hiyo.
Mh.
Mavunde amesema hadi kufikia mwezi february mwaka 2018 jumla ya wafanyabiashara
3486 wa dawa za kulevya wamekwisha kufikishwa mahakamani na kati ya hao zaidi
ya asilimia 30 ni wafanyabiashara wakubwa.
Naibu
Waziri Mavunde amesema Serikali imejitahidi kutoa elimu kwa waathirika wa
matumzi ya dawa za kulevya na hadi kufikia mwezi february 2018 waraibu wapatao
5560 wameendelea kupata tiba katika vituo 5 vya Serikali na lengo ikiwa ni
kusambaza huduma hiyo Nchi nzima ili kuwafikia waraibu wengi zaidi.
Kwa
upande wake Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri mkuu sera, bunge, kazi vijana na
wenye ulemavu Mh. Jenista Mhagama amewataka wamiliki wa soba house Nchi nzima
kuacha mara moja kuwaweka vijana katika kambi hizo kwa faida binafisi bila
msaada maalumu.
Na Pius Jayunga
Dodoma FM
Comments
Post a Comment