
Halmashauri ya
Manispaa ya Dodoma imeishukuru serikali
kupitia Wizara ya Elimu kwa kuipatia fedha kwa ajili ya kuimarisha miundombinu
ya Shule mbalimbali za Manispaa hiyo chini ya Mradi wa lipa kwa Matokeo.
Afisa Elimu
Sekondari wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma Mwl. Mwisungi Kigoso ameshukuru
wakati alipotembelea shule mbili za Nkuhungu na Chang’ombe ambazo kila moja
imejengewa madarasa manne kwa fedha za Mradi huo.
Mw. Kigosi amesema
kiasi cha fedha shilingi milioni 993.1 zilizotolewa sitasaidia kutekeleza
miradi mbalimbali ya shule ikiwemo kukusanya takwimu mbalimbali, kuhamisha
walimu kwenda katika shule nyingine pamoja na kujenga madarasa na vyoo.
Amesema mradi huo
umekuwa ni Mkombozi kwa shule kwa kuimarisha miundombinu na kujenga madarasa
kutokana na kuwepo kwa idadi kubwa ya wanafunzi iliyopelekea upungufu wa
madarasa.
Nao baadhi ya
wanafunzi walionufaika na Mradi huo wameishukuru serikali kwa kuwatatulia
changamoto zinazowakabilihususani za miundombinu ya madarasa pamoja na vyoo.
Na Phina Nimrod
Dodoma FM
Comments
Post a Comment