Jeshi la polisi Mkoani Dodoma kitengo
cha usalama barabarani limewataka madereva wa usafiri wa UMMA kutenga muda
wa kupumzika kabla ya kuanza safari na kuepuka kuzungumza na Simu.
Rai
hiyo imetolewa leo na mkaguzi msaidizi wa polisi mkoani Dodoma Josephat Mjema
wakati akizungumza na Dodoma FM ambapo amesema dereva anapokuwa kwenye safari anapaswa kuacha
mazungumzo na wasaidizi au abiria wake na badala yake azingatie kanuni na
taratibu barabarani.
Kamanda
Mjema amesema dereva anapojua kuwa kesho
ana safari anapaswa kujihakikishia anapata
muda wa kupumzika kabala ya kuanza safari ili kumsaidia kuwa makini awapo
safarini na kuepusha ajali ziazoweza kujitokeza .
Akizungumzia
malalamiko ya baadhi ya madereva juu ya ukamataji wa vyombo vya moto hususani
bodaboda Kamanda Mjema amekiri kuwepo kwa malalamiko ambapo amesema kuwa jambo hilo halina ukweli wowote kwani jeshi
la pilosi liliunda kikosi kazi kwa ajili ya zoezi hilo baada ya kuonekana uwepo
wa ukiukwaji wa sheria kama kushindwa
kusimama pindi wanaposimamishwa.
Hata
hivyo Kamanda Mjema amesema kwa sasa ajali za Bodaboda zimepungua kwa kiasi
kikubwa ukilinganisha na mwaka jana kwani awali zilikuwa zikitokea ajali 3 mpaka
4 kwa siku moja na kwa sasa imekuwa ikitokea ajali moja ama isitokee kabsa
ndani ya wiki nzima.
Na
Alfred Bulahya Dodoma Fm
Comments
Post a Comment