Maaskofu
na watumishi wa dini nchini wameshauriwa
kuacha kuingia kwenye masuala ya kisiasa yanayochochea kuleta malumbano kwa
jamii na badala yake wajikite kutatua
migogoro iliyopo nchini.
Ushauri huo
umetolewa leo na askofu mkuu wa makanisa ya pentekoste mjini Dodoma ambaye pia
ni mwenyekiti wa umoja wa madhehebu ya kikirsto mkoa wa Dodoma askofu Damas
Mukassa wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa.
Amesema kuwa nchi
ya Tanzania bado ina changamoto nyingi zinazopaswa kushughulikiwa hivyo ni
vyema watumishi wote wa dini wakaachana na mambo yanayokinzana na shughuli
zinazochangia kuleta maendeleo kwa jamii bali
waunge mkono juhudi zinazofanywa na serikali ya awamu ya tano ili
kuendelea kukuza uchumi wa nchi na hasa uchumi wa viwanda.
Askofu Mukassa amewataka
pia kuacha kulalamikia ugumu wa maisha wakidai serikali imebana pesa bali
wafanye kazi mbalimbali zinazoweza kuwaingizia vipato pamoja na kutekeleza
majukumu yao waliyopewa na taasisi zao kama kukemea masuala ya uovu na ufisadi .
Katika hatua
nyingine askofu Damas amelaani na kupinga vikali taarifa zinazosambazwa
mitandaoni za kutaka wananchi wanafanye maandamano mnamo april 26 mwaka huu
kwani madai yanayodaiwa hayana tija kwa taifa ambapo amewaomba wananchi kupuuza
taarifa hizo huku pia akiviomba vyombo vya dola kusimama imara ili kuhakikisha jambo
hilo halitokei.
Na Alfred Bulahya Dodoma
FM
Comments
Post a Comment