
Kiwango cha
maambukizi ya ugonjwa wa Malaria
nchini kimeshuka kwa nusu zaidi
kutoka asilimia 14.4 mwaka 2015 hadi kufikia asilimia 7.3 mwaka 2017.
Hayo yamebainishwa Leo na
Waziri wa Afya maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Mh. Ummy Mwalimu wakati wa maadhimisho ya
siku ya malaria Duniani ambayo kwa Tanzania Kitaifa yamefanyika Wilayani Kasulu Mkoani Kigoma.
Waziri UMMY amesema
kuwa ili watanzania tuendelee kutokomeza
ugonjwa wa malaria watanzania wanatakiwa kushiriki kikamilifu katika
kutumia afua zote za kupambana na ugonjwa huo ikiwemo kunyunyizia viuadudu vya
kuua viluilui vinavyoweza kuleta malaria.
Vilevile waziri
Ummy amesisitiza kuwa kila halmashauri za kila wilaya kuunda kamati zitakazo
hamasisha usafi wa mazingira ili kuondoa
mazalia ya mbu katika kutokomeza malaria
Sambamba na hilo Mh.UMMY amezindua takwimu za ugonjwa wa malaria nchini ambao umefanywa na Taasisi
ya takwimu NBS ambayo ndiyo takwimu itakayotumiwa na serikali ya Tanzania
Kwa upande wake
waziri wa elimu na ufundi Prof Joyce Ndalichako amesema kuwa atahakikisha wanafunzi wanapambana na ugonjwa wa malaria
kwa kuweka somo la afya kwa shule zote za msingi na sekondari nchini.
Kilele cha
maadhimisho ya siku ya Malaria Duniani kimefika tamati leo kwa kufanyika
katika wilaya ya Kasulu Mkoani KIGOMA ikiwa yamebeba kauli mbiu isemayo NIPO TAYARI KUTOKOMEZA MALARIA WEWE JE..?
NA
LUCAS GODWIN CHANZO :WIZARA YA
AFYA
Comments
Post a Comment