Kufuatia kutungwa kwa sheria
mpya namba 5 ya mwaka 2015 ya kudhibiti
na kupambana na dawa za kulevya nchini imechangia kwa kiasi kikubwa kuongezeka
kwa kasi ya mapambano ya kudhibiti dawa hizo.
Naibu
waziri wa ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na watu wenye ulemavu
Mh. Athony Mavunde ameyasema hayo leo Bungeni Mjini Dodoma wakati akijibu swali
la Mbunge wa viti maalumu Mwantumu Dau Haji aliehoji ni hatua zipi
zimechukuliwa katika mapambano ya kudhidhiti biashara ya dawa za kulevya.
Mh.
Mavunde amesema sheria hiyo imeipa Serikali mamlaka makubwa ya kuanzisha chombo
cha kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya kilichoundwa mwaka 2017 kikiwa na
mamlaka ya kukamata, kupekua, kuzuia mali na kuchunguza mashauri yote ya dawa
za kulevya.
Amesema
katika kuongeza kasi dhidi ya mapambano ya dawa za kulevya mwaka, 2017
yalifanyika marekebisho madogo katika sheria hiyo na kuipa mamlaka mara dufu
ambapo katika kipindi cha mwaka mmoja hadi kufikia February 2018 watuhumiwa
11,071 walikamatwa wakiwemo watuhumiwa 3486 ambao ni wafanyabiashara wa dawa za
kulevya.
Awali Naibu Spika Mh. Tulia
Ackson, ameongoza zoezi la kuwaapisha wabunge wawili, Dk Godwin Mollel wa jimbo
la Siha na mbunge Maulid Mtulia wa jimbo la Kinondoni baada ya kufanyika kwa
uchaguzi mdogo katika majimbo hayo kufuatia wabunge wa maeneo hayo kuhamia
Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Comments
Post a Comment