Kampeni ya kufanya
usafi kila jumamosi imesaidia kupunguza baadhi ya magonjwa mkoani Dodoma ikiwemo malaria na magonjwa ya mlipuko pamoja na magonjwa ya matumbo.
Bwana Aleck
Barankena ni afisa afya manispaa ya Dodoma ameiambia Dodoma Fm kuwa suala la
kufanya usafi kila jumamosi limesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza magonjwa
hayo kutokana na watu kusafisha maeneo yao kikamilifu.
Amesema jamii
inapaswa kubadilika na kuacha kusubiri kusimamiwa katika suala la usafi hasa
katika kipindi hiki cha mvua ili kuzuia mbu kuzaliana na kusababisha malaria
pamoja na mlipuko wa magonjwa ya matumbo.
Barankena amewataka
viongozi katika ngazi za mtaa ,kata na tarafa kushirikiana na viongozi wa
manispaa katika kuhimiza suala la usafi ikiwa ni pamoja na matumizi ya choo bora.
Kampeni ya kufanya
usafi iliasisiwa na Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tangazania na kutangaza
kila jumamosi ya mwisho wa mwezi watu kuitumia kufanya usafi na kwa mkoa wa Dodoma kampeni hiyo imeendelezwa na imezaa matunda.
Mariam
Matundu Chanzo Dodoma FM
Comments
Post a Comment