
ukwaa la wakulima la
wanawake Wilaya ya Chamwino (JUWACHA) lililopo chini ya shirika lisilo la
kiserikali la Action Aid limeiomba serikali
kuongeza jitihada katika sekta ya afya kutokana na zahanati ya Mlodaa
kukabiliwa na upungufu wa wahudumu,madaktari, pamoja na dawa.
Hayo yamebainishwa na mwenyekiti wa Jukwaa hilo Bi. Janeth
Nyamayahasi wakati akiwasilisha taarifa ya matokeo ya tathmini ya pima kadi
kuhusu huduma za jamii.
Amesema sekta ya afya inakabiliwa na changamoto ikiwa ni pamoja
na upungufu wa zahanati katika kata mbalimbali na nyingine kukabiliwa na
upungufu wa wahudumu, madaktari, pamoja na dawa hali inayopelekea jamii
kutopata matibabu kwa ubora.
Kwa upande wake Afisa
Maendeleo ya Jamii kutoka Chamwino Andrew Kayamgoya amesema ni kweli matatizo
hayo yapo ikiwemo uhaba wa watumishi kwenye idara ya afya unaochangiwa na
kustaafu kwa baadhi ya watumishi , pamoja na kuhamishiwa sehemu nyingine.
Matokeo ya tathmini
hiyo yamefanyika Katika kata nane za wilaya ya Chamwino ikiwemo Mlowa
Barabarani, Iringa Mvumi, Makang’wa, Buigiri, Chamwino, Msanga,Chilonwa Na
Machali ambayo yamefanywa na Jukwaa la wakulima wanawake wilayani hapo JUWACHA
lililopo chini ya shirika lisilo la kiserikali la ACTION AID.
Na,Mindi
Joseph Dodoma FM
Comments
Post a Comment