Jeshi la polisi
mkoa wa Dodoma limewakamata wahamiaji haramu saba ambao sita kati yao ni
wasomali wenye uraia wa Kenya walioingia nchini Tanzania bila kibali halali.
Akizungumza na
waandishi wa habari mapema hii leo Kamanda wa polisi mkoani hapa GILLES MUROTO
amesema Uchunguzi wa awali unaonekana wahamiaji hao wanaingia nchini kupitia mpaka wa
Namanga-ARUSHA na hati zao zimegongwa mihuri inayo tofautiana na kutiliwa
mashaka kuwa sio hati halali.
Kamanda MUROTO
amewataja wahamiaji haramu kuwa ni Mussa Abdi Isaka mwenye umri wa miaka 37,
Aden Awes Abdi 34, John Gichuchi Mbogo 28,Abraham Hussein Ismail 22, Joseph
Mbuthia Kibuko 33,Mohamed Abdi Kosar 28
wote wakiwa ni Raia wa kenya wamekamatwa kwenye basi la kampuni ya
NGASERE lenye namba T.675 DJT linalofanya safari zake kati ya Mpwapwa na
Iringa.
Wakati huo huo Jeshi
la polisi limefanikiwa kukamata watu wawili ambao ni wavunjaji wa nyumba na
kuiba mali mbalimbali za wizi ambazo ni Laptop 2 aina ya lenovo na Sony ,
Desktop computer 1 aina ya Dell, Flat screen TV aina ya Samsung watuhumiwa hao
wakiwa ni Beda Nathaniel 31 , Dickson Mrisho 27 wanaofanya kazi ya ujenzi na ni
wakazi wa Makuru Dodoma.
Kamanda MUROTO
amesema wahalifu wengi wa uvunjaji ni mafundi ujenzi hivyo ametoa tahadhari kwa
wananchi wa Dodoma kuchukua tahadhari ya mafundi kwa kuwa ndio wanaorudi
kuvunja na kuiba baada ya kujenga wenyewe.
Sambamba na hayo
Jeshi la polisi linawapongeza watoa Taarifa kwa kutambua uhalifu na kuchukua
hatua mapema kwa kutoa Taarifa kwa jeshi la polisi na kuwataka wamiliki na
wafanyakazi katika vyombo vya Usafiri wasikubali kuingia matatizoni kwa
kusafirisha wahamiaji haramu kwa kuwa magari yao yatataifishwa kwa mujibu wa
sheria.
Na
ANIPHA RAMADHAN DODOMA FM
Comments
Post a Comment