Naibu waziri wa
afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto FAUSTINE NDUNGURILE amezitaka
hospitali zote za watu binafisi kuwa na
leseni za kuendesha hospitali hizo kwa lengo la kuendeleza mfumo bora wa utoaji
wa huduma kwa jamii.
Akizungumza na
waandishi wa habari mapema leo katika uzinduzi wa bodi mpya ya ushauri wa
hospitali za watu binafisi ambao umeambatana na uzinduzi wa kanuni mpya za
hospitali binafisi,viwango vipya vya takwimu pamoja na Tehama amesema lengo
kubwa la uzinduzi huo ni kuhakikisha hospitali binafisi zinakuwa na leseni za
utoaji huduma kwa jamii.
NDUGURILE ameongeza
kuwa suala la kuwa na leseni ni la muhimu kwa hospitali zote za umma hivyo
hospitali za watu binafisi zinatakiwa
kufuata kanuni za kuwa na leseni ili
kuendana na mfumo bora wa utoaji wa huduma.
Katika hatua
nyingine Ndungurile amebainisha sekta ya afya tayari imefanikiwa kuboresha
huduma za afya 208 za kutolea afya ikiwemo nyumba za maabara,Chumba cha
kujifungulia mama wajawazito pamoja na
nyumba za watumishi.
Aidha wizara ya afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na
watoto kwa mwaka huu wa fedha 2018/19 inatarajia kujenga hospitali za wilaya 67
kwa lengo la kuwafikia wananchi wote.
Na,Mindi
Joseph Dodoma FM
Comments
Post a Comment