Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetaja
changamtoto tano za uendeshaji kesi zinazotokana na makosa ya mtandao.
Changamoto hizo zimetajwa kuwa ni uelewa mdogo wa majaji,
mahakimu na wanasheria, ushahidi wa kuwasilisha, kufutika kirahisi, uchunguzi,
na wapi pa kupeleka malalamiko hayo.
Mwanasheria mwandamizi kutoka TCRA, Dk Philip Philikunjombe
amewataka majaji na mahakimu na wanasheria kupata elimu juu ya uendeshaji wa
kesi hizo kwani kumekuwa na makosa makubwa yanayotendeka.
Mbali na hiyo amesema bado kuna ugumu wa kujua ni namna gani
ushahidi unatakiwa kuwasilishwa mahakamani pindi mtu atakapokwenda kulalamika
kuwa katendewa makosa.
Lakini pia changamoto nyingine ni ushahidi wa kesi hizo
kuharibika kirahisi kwa sababu mtuhumiwa anaweza kufuta ujumbe hivyo haitakuwa
rahisi kuthibitisha makosa hata kama ujumbe huo utakuwa nao mlalamikaji.
Kufuatia changamoto hizo wadau mbalimbali wanaotumia mitandao
wameshauri wasimamizi wa kesi hizo kupewa elimu ya sheria zinazohusu makosa ya
mtandao ili haki iweze kutendeka.
NA LUCAS GODWIN
Comments
Post a Comment