Jamii imeshauriwa
kuacha kuwatumia watoto wakike wenye umri wa kwenda shule kama kitega uchumi
kwa kuwaozesha wakiwa na umri mdogo, badala yake ishiriki kwa pamoja kupinga
ndoa za utotoni.
Wito huo umetolewa
huku zikiwa zimepita siku chache, mara baada ya mtoto mwenye umri wa miaka kumi
na saba kuikimbia familia yake huko mkoani Manyara na kukimbilia mkoan Dodoma
sababu ikiwa ni kukataa kuolewa akiwa na umri mdogo.
Akiongea na kituo
hiki kwa masikitiko mtoto huyo amesema ameamua kuikimbia familia yake iliyopo
kijiji cha Basuto mkoani Manyara kwa kulazimishwa na mjomba wake aolewe, mjomba
aliyekuwa akimlea mara baada ya mama yake kufariki.
Akieleza namna alivyompata mtoto huyo, mama anayeishi na mtoto huyo katika kata ya Mnadani
Manispaa ya Dodoma amesema mtoto huyo alifika kwake na kueleza
matatizo yaliyompata na ndipo akatoa taarifa kwenye uongozi wa eneo hilo.
Kwa upande wake
diwani wa kata ya Mnadani Bi Farida Mbaruku amesema wameipokea taarifa kwa masikitiko na kuahidi
kufanya jitihada za mtoto huyo kusaidiwa huku akionya watu wenye tabia kama hizo
kuacha kwani atakayebainika atachukuliwa hatua za kisheria.
Na
Victor Makwawa DODOMA FM
Comments
Post a Comment