
Producer na msanii kutoka studio ya Destination sound Dodoma Binladen amesema aliacha kurap kutokana na kuanzisha kundi la C.M.A ambapo nafasi yake ilichukuliwa na Gifted Son.
Amesema kundi hilo lina ndoto kubwa ili kuutangaza mziki wa rap nchini na nje ya mipaka ya Tanzania ukitofautisha na mziki wa kuimba.
Amemtaja Teidy Wizy kutoka kundi hilo kama mwanamke ambaye anajua kuchana tofauti na rapa yeyote wakike nchini endapo atajiamini.
Katika hatua nyingine msanii huyu amesema anampango wa kurudi tena katika nafasi yake huku wengi wakiamini anauwezo wa kutengeneza nyimbo pekee.
Hata hivyo kundi hilo linaundwa na watu watatu ambao ni Binladen,Miracle pamoja na Tedy wizzy
Na Beny Bert
Comments
Post a Comment