ASILIMIA 37 YA WATOTO HUZALIWA NA MATATIZO YA UTINDIO WA AKILI,MGONGO WAZI NA VICHWA VIKUBWA MJINI DODOMA
Baadhi ya mikoa
nchini Tanzania imegundulika kuwa na
changamoto ya kuzaliwa kwa watoto wenye mtindio wa akili,mgongo wazi, pamoja na
kuzaliwa na vichwa vikubwa na hii ni kutokana na kinamama wajawazito
kutozingatia mlo kamili wawapo katika kipindi cha ujauzito.
Hayo yamebainishwa
na Afisa lishe Mkoa wa Dodoma Bi.Mariam Mwita wakati akizungumza na Dodoma FM
ambapo amewataka kinamama wajawazito kuwekeza katika siku elfu moja (1000)tangu
mimba inapotungwa,Mtoto anapozaliwa hadi
pale mtoto atakapofikisha miaka miwili.
Katika mkoa huu wa
Dodoma imeonekana kuwa Tatizo hili la kuzaliwa kwa watoto wenye mtindio wa
akili lipo kwa asilimia 37 jambo ambalo linapelekea kuongezeka kwa watoto wa
mtaani kutokana na watoto hao kutokuelewa
masomo wakiwa darasani na kusababisha kukimbia shule.
Pia amefafanua kuwa
Tatizo la kuzaliwa kwa watoto wenye
kasoro kimaumbile linaanzia pale mimba inapotungwa bila mama kujiandaa na hivyo
kuwataka kinamama kutumia vidonge vya FOLIC ACID ambavyo vinamkinga mtoto
kupatwa na maambukizi ya mangonjwa mbalimbali .
Aidha Bi. Mwita
ametoa ushauri kwa wazazi kunyonyesha watoto wao kwa kipindi cha miaka miwili
na nusu kutokana na lishe inayopatikana katika maziwa ya mama ambayo inamjengea afya mtoto huyo tofauti na vyakula
vingine ambavyo vinaweza vikamsababishia kuugua utapiamlo.
Na
ANIPHA RAMADHAN CHANZO:DODOMA FM
Comments
Post a Comment