Wahitimu wa kidato cha sita katika shule ya sekondari Dodoma wametakiwa kuhakikisha wanaitumia vizuri elimu waliyoipata kwa kuwa mabalozi wakubwa katika kusaidia ujenzi na ustawi wa taifa ili kuleta mabadiliko chanya katika jamii.
Kauli hiyo imetolewa leo na Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde wakati akitoa hotuba kwa wanafunzi wa shule ya sekondari Dodoma katika mahafali ya 15 ya kidato cha sita yaliyofanyika mapema hii leo shuleni hapo.
Mavunde Amesema kuwa wahitimu hao wanatakiwa kuwa mabalozi wazuri kwenye jamii katika kutoa elimu juu ya maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi pamoja na madhara ya matumizi ya madawa ya kulevya ambayo yamekuwa yakichangia kuongeza kundi kubwa la watu wenye utegemezi.
Awali akisoma risala mbele ya mgeni rasmi mkuu wa shule ya sekondari Dodoma Amani Mfaume ameiomba serikali kuhakikisha inatatua changamoto ya upungufu wa mabweni kwa ajili ya wanafunzi wa kiume kwani jambo hilo limekuwa likisababisha baadhi ya wanafunzi kupanga vyumba mitaani hali ambayo inawafanya kukosa usimamizi katika masomo na kusababisha kuwa na ushiriki hafifu kwenye masomo yao.
Amesema mbali na hilo baadhi ya wanafunzi wamekuwa wakijikuta wakiingia katika vishawishi mbalimbali vya kuishi katika maisha ya kimjini na kusababisha matokeo yao kuwa mabaya ukilinganisha na upande wa wasichana ambao wanaishi ndani ya eneo la shule.
Aidha Mavunde ameahidi kuhakikisha changamoto hizo zinatatuliwa katika shule hiyo ili kuwajengea uwezo mkubwa wa kitaaluma wanafunzi hao.
Na Alfred Bulahya.

Comments
Post a Comment