Zoezi la uandikishaji wa vitambulisho vya Taifa NIDA katika awamu ya tano limefikia tamati kwa
kata ya KIZOTA na NKUHUNGU mjini Dodoma huku
baadhi ya wananchi wakiwa bado hawajajiandikisha.
Wananchi ambao hawajajiandikisha wametakiwa kuandaa nakala
pamoja na viambatanisho vyao ili kuondoa usumbufu unaojitokeza.
Akizungumza na kituo hiki Afisa usajili wa mamlaka ya
vitambulisho vya taifa NIDA Mkoa wa
Dodoma KHALID MRISHO amesema changamoto
kubwa ni wananchi kutokuwa na viambatanisho vya kuwatambulisha na Zoezi hilo lilianza tarehe 16 mwezi huu na limefika tamati leo kwa kata hizo.
Amesema hadi kufikia jana watu wapatao 1,771,300 walikuwa
wamesajili na zoezi hilo ni endelevu
katika kata mbalimbali kwa mkoa wa Dodoma.
Kwa upande wake afisa mtendaji wa kata amewataka wananchi
kuendelea kutambua umuhimu wa vitambulisho vya uraia kwa sababu baadhi yao
wamekuwa wakidai havina umuhimu wowote.
Baada ya kukamilika katika awamu ya tano ambayo imehusisha
kata mbili na litaendelea katika awamu ya sita kwa kata ya CHANGOMBE na CHAMWINO kuanzia jumamosi huku watu
takiribani 24,000 elfu wakitarajia kusajiliwa.
Na,Mindi Joseph Dodoma
FM
Comments
Post a Comment