Msanii
wa mziki wa kizazi kipya kutoka Dodoma Zipora ameilaumu jamii kutokana na kutoa
nafasi kubwa kumsapoti mwanaume huku mwanamke akiachwa nyuma.
Ziporah ni ni miongoni mwa wasanii wa kike ambao wanatajwa mara
nyingi kwa kuwa na kipaji cha mziki pamoja na sauti nzuri ya uimbaji.
Akizungumza na Beat Drive Show amesema jamii kubwa ya kiafrika
inatoa nafasi kubwa kwa mwanaume bila kujua kuwa mwanamke ananafasi kubwa na
anaweza kufanya zaidi ya kile ambacho mwanaume anaweza kufanya.
Akizungumzia kuhusu kuwepo kwa wasanii wachache wakike mkoani
Dodoma amesema baadhi yao ni waoga na baada ya kufanya kazi chache hawaoni
umuhimu wakuendelea kufanya kazi hiyo ili waendelee kuongeza ukubwa wa majina
yao.
Hata hivyo ametoa ushauri kwa watayarishaji wa mziki mkoani Dodoma
kutokuridhika hivyo kuongeza juhudi na jitihada ili waongeze ukubwa wa kazi
zao.
Ameongeza kuwa kwa mwaka 2018 ana mikakti ya kuongeza ukubwa wa
kazi zake ikiwa ni pamoja na kufanya kazi na watayarishaji wa mziki kutoka nje
ya mkoa wa Dodoma.
Na Beny Bert
Comments
Post a Comment