Mkuu
wa wilaya ya chemba mkaoni Dodoma bwana Simon Odunga amezilalamikia kamati za
mazingira katika wilaya yake kwa kuto kuwajibika ipasavyo hali iliyosababisha
zaidi ya watu elfu nne kukosa makazi mpaka sasa kutokana na mafuriko.
Bwana Odunga
ameyasema hayo wakati akizungumza na DODOMA FM HABARI juu ya tatizo la mafuriko lililopelekea
kuezuka kwa nyumba kadhaa huku wananchi wakikosa makazi.
Mkuu huyo wa wilaya
ameonekana akisikitishwa na utendaji kazi wa kamati za mazingira kuanzia ngazi
ya wilaya mpaka ngazi ya kijiji.
Amesema amekuwa
akihamasisha kamati hizo pamoja na wananchi kuto kuharibu mazingira ikiwemo
kufanya shughuli za kilimo milimani lakini tatizo ni kamati hizo kushindwa
kufanya ufuatiliaji.
Hata hivyo amesema
kamati hizo zimekuwa zikifanya kazi kinyume cha taratibu kwani wakati mwingine
anapobainika mtu anahusika na uharibifu wa mazingira na kupelekwa kwenye vyombo
vya sheria kamati hizo zimekuwa zikiwatetea jambo ambalo halitakiwi.
Bwana Odunga
amesema kuna mpangango mpya ambao wameanzisha kwa sasa wa kuhakikisha
wanarejesha uoto wa asili katika eneo la mrijo ambalo limeathirika na mafuriko
na kuwataka waathirika wa mafuriko hayo kuhama haraka iwezekanavyo.
Mapema mwezi wa
February yaliripotiwa mafuriko katika wilaya ya Chemba eneo la mrijo mkoani
Dodoma yaliyosababishwa na mvua hali iliyopelekea kuanguka kwa kaya 570 mpaka
sasa.
Na
Benard Filbert
Dodoma FM
Comments
Post a Comment