
Kiungo
wa Manchester City, Yaya Toure, ameondolewa katika kikosi cha timu ya
taifa ya Ivory Coast ambacho kinatarajia kucheza mchezo wa kirafiki
dhidi ya Togo na Moldova.
Kwa mujibu wa BBC, Toure ameondoshwa kikosini kutokana na sababu za kifamilia.
Toure
alikuwa anarejea tena kuitumikia timu yake ya taifa baada ya kufuta
uamuzi wake alioutoa 2015 kipindi cha Michuano ya Kombe la Mataifa ya
Afrika wa kutaka kustaafu kuichezea.
Ivory Coast itakuwa na kibarua dhidi ya Togo Machi 24 na dhidi ya Moldova 27 Machi 2018.
Comments
Post a Comment